Orodha ya makampuni ya kilimo cha mazao ya chakula nchini Tanzania na Gine-Bisau ili kukuza biashara yako

Digitalfem

Mradi wa “Kipindi cha mpito wa kidijitali, mshikamano wa kijamii na usawa wa kijinsia: huduma za kibenki kwa njia ya simu na uwezeshaji wa wanawake kidijitali barani Afrika” (DIGITALFEM), wenye Kumbukumbu Na. TED2021-130586B-I00, ni sehemu ya Miradi ya Vipindi vya Mpito wa Kiikolojia na Mpito wa Kidijitali (Wizara ya Sayansi na Ubunifu ya Serikali ya Hispania), ambayo Mtafiti Mkuu wake ni Roser Manzanera Ruiz (Idara ya Sosholojia na Taasisi ya Chuo Kikuu ya Taaluma za Wanawake na Jinsia, Chuo Kikuu cha Granada) na Mtafiti Mkuu-Mwenza ni Soledad Vieitez Cerdeño (Idara ya Anthropolojia ya Jamii na Taasisi ya Chuo Kikuu ya Taaluma za Wanawake na Jinsia, Chuo Kikuu cha Granada). Inafadhiliwa na MCIN/AEI/ 10.13039/501100011033 na “Mfuko wa Umoja wa Ulaya wa NextGenerationEU/PRTR” kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Desemba 2022 hadi Novemba 30, 2024.

Huu ndio mradi pekee uliopata tuzo katika Sayansi za Jamii katika uga wa Taaluma za Kifemisti, ambao utafiti wake unashughulikia michakato ya kijamii ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika kipindi cha mpito wa kidijitali wa wajasiriamali wa kike katika sekta ya kilimo cha mazao ya chakula katika maeneo ya mijini yenye tamaduni mchanganyiko za Gine-Bisau na Tanzania. Kimahususi, mradi huu unapendekeza kutambuliwa na kuhifadhiwa kwa mikakati ya kifedha ya kidijitali ya wanawake (kwa mfano, matumizi ya teknolojia ya simu katika utendaji wao wa kiuchumi), ndani ya mfumo wa miktadha yao mahususi ya kitamaduni, na kwa kujikita katika uhusiano changamani baina ya teknolojia, jinsia, maendeleo, uchumi, na siasa za kijamii.

Taarifa zaidi zinapatikana kwenye tovuti ya kikundi cha utafiti ya AFRICAInEs research group (SEJ-491) na ya 1st International Conference “Social Sciences and Digital Humanities: Cooperation, Cultures, Societies and African Processes of Digitalization in Sub-Saharan Africa”.(Kongamano la Kwanza la Kimataifa la “Sayansi za Jamii na Insia za Kidijitali: Ushirikiano, Tamaduni, Jamii na Michakato ya Udijitishaji barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara”).