1. Taarifa za jumla
Tovuti hii inamilikiwa na Chuo Kikuu cha Granada chenye anwani iliyosajiliwa ya Rector Lopez Argüeta s/n 1801 Granada (HISPANIA), na namba ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) Q1818002F. Kwa maulizo yoyote, unaweza kuwasiliana nasi kwa anwani ya baruapepe digitalkifem@gmail.com
2. Masharti ya Matumizi
Kuingia katika tovuti hii na kuitumia kunategemea masharti yafuatayo. Kwa kuingia katika tovuti hii na kurasa zake zozote, unakubali kuzingatia na kubanwa na vigezo na masharti yaliyoainishwa hapa chini.
3. Milki Dhihini
Maudhui yote kwenye tovuti hii, ikiwa ni pamoja na maandishi, michoro, picha, nembo, ikoni, maunzilaini na mengineyo, ni mali ya [Jina la Kampuni] au watoa leseni wake na yanalindwa na sheria za milki dhihini. Utoaji upya, usambazaji, uwasilishaji kwa umma, na ubadilishaji wa maudhui haya ni marufuku bila kupata idhini kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Granada.
4. Ukomo wa Kuwajibika
Chuo Kikuu cha Granada hakiwajibiki na uharibifu wowote au madhara ya aina yoyote yanayoweza kutokea kutokana na mtumiaji kuingia katika tovuti hii au kuitumia, ikiwa ni pamoja na makosa au udondoshaji wa maudhui, kutopatikana kwa tovuti, au kusambaa kwa virusi au programu zenye madhara au uharibifu wa mauhdui, licha ya kuchukua hatua zote muhimu za kiteknolojia za kuyazuia hayo.
5. Viungo vya Wahusika Wengine
Tovuti hii inaweza kuwa na viungo vya tovuti nyingine zinazoendeshwa na wahusika wengine. Chuo Kikuu cha Granada hakiwajibiki na maudhui au hali ya tovuti hizi. Utumiaji wa tovuti hizi utakuwa chini ya vigezo na masharti ya matumizi yaliyowekwa katika kila moja ya tovuti hizo.
6. Ulinzi wa Taarifa Binafsi
Kwa mujibu wa kanuni zilizopo za ulinzi wa taarifa binafsi, Chuo Kikuu cha Granada kinaahidi kuchukua hatua za kiufundi na za kitaasisi zinazohitajika ili kuhakikisha usalama wa taarifa binafsi na kuzuia kubadilishwa, kupotezwa, kuchakatwa au kufikiwa kwazo bila idhini.
7. Sheria na Mamlaka Zinazohusika
Masharti haya yanasimamiwa na sheria za Hispania. Kwa utatuzi wa migogoro yoyote inayoweza kujitokeza kuhusiana na uhalali, utekelezaji, uzingatiaji, au usitishaji, kikamilifu au kwa sehemu, wahusika watawasilisha, wakiziachia mamlaka za Mahakama na Mabaraza ya Granada (Hispania) mamlaka yao wenyewe au nyingine yoyote ambayo inaweza kufungamana nao.
8. Marekebisho ya Taarifa za Kisheria
Chuo Kikuu cha Granada ndicho chenye haki ya kurekebisha taarifa hizi za kisheria ili zilingane na maendeleo ya kisheria pamoja na mienendo ya tasnia inayohusika. Katika mazingira kama haya, Chuo Kikuu cha Granada kitatangaza kwenye ukurasa huu mabadiliko yaliyofanywa kwa kutoa taarifa mwafaka kabla ya kutekelezwa.